Tuesday, 6 September 2016

SIMBA SPORTS CLUB VPL LEO
Simba sports club ya jijini Daresalaam itawakaribisha Ruvu shooting stars ya Mlandizi Pwani katika raundi ya tatu ya michuano ya ligi kuu Tanzania Bara yani (VPL) .
Mchezo huo utapigwa majira ya saa kumi jioni katika uwanja wa Uhuru Dar es salam leo tarehe 7/9/2016.
Msemaji wa timu ya Ruvu shooting Bwana Masau Bwire amejigamba kua timu yake ipo vizuri na simba wategemee kipigo kikali.
Aidha msemaji wa klabu ya Simba ndugu Haji Manara amesema yeye hana Mbwembwe bali ataongea baada ya mechi kumalizika.
Simba watashuka dimbani wakiwa na kumbukumbu ya kubanwa mbavu na maafande wa Jkt ruvu baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana katika raundi ya pili ya ligi hiyo , huku wenzao Ruvu shooting wakiwa na kumbukumbu ya kuchapwa na Tanzania prisons ya Mbeya.

No comments:

Post a Comment