Wednesday, 7 September 2016

SIMBA SC NA AZAM WAFANYA KWELI ,YANGA JINAMIZI LA REKODI MBAYA NANGWANDA SIJAONA LAENDELEA

Timu za Simba sports club na Azam football club zimetamba katika mechi zilizopigwa leo majira ya saa kumi jioni.
Katika michezo hiyo Simba waliinyuka Ruvu shooting stars mabao mawili kwa moja , Ruvu shooting walikua wakwanza kuandika bao mapema lakini simba walijibu dakika mbili baadae kwa kusawazisha bao hilo kupitia kwa mchezaji mashuhuri Ajibu.
Dakika ya 46 mshambuliaji wa kimataifa wa simba Laudit Mavugo alipachika bao la pili baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Ajibu.
Na mpaka Dakika tisini zinamalizika simba walikua mbele kwa bao 2 kwa 1.
Katika Mchezo mwingine uliopigwa huko Mbeya katika Uwanja wa Sokoine Azam wanalambalamba kutokea chamazi Dar es salaam waliinyuka Tanzania prisons Bao moja kwa bila
                                       AZAM 1 -T.PRISONS 0

Na huko Nangwanda sijaona Yanga wameshindwa kutamba mbele ya Ndanda FC kwa kulazimishwa sare ya bila kufungana.
                                       YANGA 0-NDANDA FC 0

Tuesday, 6 September 2016

MECHI VPL LEO TAREHE 7/9/2016

Ndanda vs Yanga sc - Nangwanda sijaona stadium
Simba sc vs Ruvu shooting -Uhuru stadium
Prisons vs Azam Fc -Sokoine Stadium




SIMBA SPORTS CLUB VPL LEO
Simba sports club ya jijini Daresalaam itawakaribisha Ruvu shooting stars ya Mlandizi Pwani katika raundi ya tatu ya michuano ya ligi kuu Tanzania Bara yani (VPL) .
Mchezo huo utapigwa majira ya saa kumi jioni katika uwanja wa Uhuru Dar es salam leo tarehe 7/9/2016.
Msemaji wa timu ya Ruvu shooting Bwana Masau Bwire amejigamba kua timu yake ipo vizuri na simba wategemee kipigo kikali.
Aidha msemaji wa klabu ya Simba ndugu Haji Manara amesema yeye hana Mbwembwe bali ataongea baada ya mechi kumalizika.
Simba watashuka dimbani wakiwa na kumbukumbu ya kubanwa mbavu na maafande wa Jkt ruvu baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana katika raundi ya pili ya ligi hiyo , huku wenzao Ruvu shooting wakiwa na kumbukumbu ya kuchapwa na Tanzania prisons ya Mbeya.

MANCHESTER DERBY

Ligi kuu ya uingereza itaendelea tena wiki hii ambapo macho ya mashabiki wengi wa mpira wa miguu yapo katika mechi kati ya Manchester united na Manchester city katika dimba la Old trafford .
mechi hii ina mvuto wa aina yake kutokana na uwepo wa makocha bora ambao wamekua mahasimu kwa muda mrefu yaani Jose Mourinho na Josep Pep Guadiola .
Na pia uwepo wa wachezaji bora katika klabu zote mbili mfano Zlatan Ibrahimovic ambaye amekua na mwanzo mzuri katika ligi ya Uingereza.
Mchezo huo utapigwa katika dimba la Old trafford mida ya saa nane na nusu mchana  siku ya jumamosi.
Mchezaji Kun Aguero ataukosa mchezo huo kutokana na adhabu aliyopewa na shirikisho la soka la nchi hiyo yani FA .


mchezaji Marcus Rashford
aliefunga bao pekee mara ya mwisho timu hizo zilipokutana

Monday, 5 September 2016

KILIMANJARO CHRISTIAN MEDICAL COLLEGE

KCMUCo
kcmuco students doing anatomy practicals in the laboratory(anatomy laboratory) at kcmuco main campus

WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KCMUCo DIPLOMA 2016/2017
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Chuo cha Afya ngazi  ya Diploma kcmuco
kuona list click link hapo chini
selected candidates for Diploma

KCMUCo

kcmuco
Moja ya vyuo bora vya afya Tanzania ,
Ni chuo kinachoendeshwa na kanisa la kilutheri Tanzania ,
hutoa kozi mbalimbali za afya kama vile ;
*Degree ya udaktari(Doctor of Medicine)
* Degree ya maabara( Health laboratory science)
* Occupational Therapy degree
*Physiotherapy degree
* Bachelor of Nursing
pia programu za diploma zapatikana chuoni hapo

 wanafunzi wakifanya mitihani kupitia mtandao wa LCMS+
 computer laboratory za kisasa kabisa


wanafunzi wakielekezwa vitu na wataalamu wa IT.

  by ..emmadeclassic

best anatomy laboratories in Tanzania

kilimanjaro christian medical college