SIMBA SC NA AZAM WAFANYA KWELI ,YANGA JINAMIZI LA REKODI MBAYA NANGWANDA SIJAONA LAENDELEA
Timu za Simba sports club na Azam football club zimetamba katika mechi zilizopigwa leo majira ya saa kumi jioni.
Katika michezo hiyo Simba waliinyuka Ruvu shooting stars mabao mawili kwa moja , Ruvu shooting walikua wakwanza kuandika bao mapema lakini simba walijibu dakika mbili baadae kwa kusawazisha bao hilo kupitia kwa mchezaji mashuhuri Ajibu.
Dakika ya 46 mshambuliaji wa kimataifa wa simba Laudit Mavugo alipachika bao la pili baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Ajibu.
Na mpaka Dakika tisini zinamalizika simba walikua mbele kwa bao 2 kwa 1.
Katika Mchezo mwingine uliopigwa huko Mbeya katika Uwanja wa Sokoine Azam wanalambalamba kutokea chamazi Dar es salaam waliinyuka Tanzania prisons Bao moja kwa bila
AZAM 1 -T.PRISONS 0
Na huko Nangwanda sijaona Yanga wameshindwa kutamba mbele ya Ndanda FC kwa kulazimishwa sare ya bila kufungana.
YANGA 0-NDANDA FC 0